𝐂𝐁𝐄 𝐒𝐀 vs 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐒𝐂
Timu ya Commercial Bank of Ethiopia Sports Association (CBE SA) ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1982.
Inapatikana mji mkuu wa Addis Ababa nchini Ethiopia.
Msimu uliopita walikuwa Mabingwa wa ligi kuu nchini Ethiopia (Ethiopian Premier League) ligi inayojumuisha jumla ya timu (16).
MAFANIKIO YA CBE SA
2023/24 - Mabingwa wa Ligi kuu nchini Ethiopia
2014 - Mabingwa wa kombe la Addis Ababa City
Timu ya CBE SA haijawahi kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika CAF Champions League na hii ni mara ya Kwanza timu hiyo inashiriki michuano ya CAFCL.
CBE SA imewahi kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho CAF confederation Cup mara mbili 2005 na 2010, haikufanya vizuri kwani mara zote hizo Waliishia hatua ya Kwanza (First Round).
TAKWIMU ZA CBE SA MSIMU ULIOPITA KUNAKO LIGI KUU NCHINI ETHIOPIA
Mechi = 30
Wameshinda Mechi = 19
Sare/Suluhu = 07
Mabao waliyofunga = 57
Mabao waliyofungwa = 27
Mechi walizopoteza = 04
Mchezo wa mkondo wa Kwanza CBE SA wakichexa dhidi ya klabu ya SC Villa na kufanikiwa kuiondosha.
CBE SA 2-1 SC Villa
SC Villa 1-1 CBE SA